02/08/2026
KATIBU MKUU WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI ATEMBELEA BANDA LA CHUO CHA VIWANDA VYA MISITU NANENANE 2026
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena, leo tarehe 02 Agosti 2026, ametembelea banda la Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo (Nanenane) yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni, jijini Dodoma.
Katika ziara hiyo, Bi. Meena alipata fursa ya kufahamu shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na chuo, ikiwemo utoaji wa mafunzo ya uhifadhi wa misitu, usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu, pamoja na teknolojia za uchakataji na uongezaji thamani wa mazao ya misitu.
Aidha, alipata nafasi ya kujionea bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na chuo kutokana na mazao ya misitu na kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha elimu na ujuzi unaochangia matumizi endelevu ya rasilimali za misitu kwa maendeleo ya taifa.