Tagamenda Poultry and Egg Incubator Construction Unit

Call Directions Website Contact the business

Tagamenda Poultry and Egg Incubator Construction Unit VIFARANGA NA VIATAMIZI

Tunauza vifaranga, na pia tunatengeneza Mashine za kuangulia vifaranga
Mashine tunazotengeneza za kuangulia vifaranga zina ufanisi mkubwa sana

SHAMBANI KWETU LEOT AN G A Z OKwa yeyote mwenye nia ya kuingia kwenye ufugaji wa kuku kibiasharq, na ana mtaji wa zaidi ...
10/09/2026

SHAMBANI KWETU LEO
T AN G A Z O
Kwa yeyote mwenye nia ya kuingia kwenye ufugaji wa kuku kibiasharq, na ana mtaji wa zaidi ya sh. 5,000,000 tuwasiliane!

27/08/2026

SHAMBANI KWETU LEO

30/07/2026

SHAMBANI KWETU LEO
UTOTOLESHAJI
Kwa wale wanaotaga kutotolesha mayai yao kwetu KARIBUNI:
ZINGATIA
1. Mayai yawe yametagwa ndani ya siku Saba
2. Mayai yawe yamerutubishwa na jogoo
3. Mayai yawe masafi ambayo umeyahifadhi sehemu isiyo na joto kupitiliza
4. Mayai yasiwe makubwa sana wa madogo sana. Yawe ya size ya kati
5. Mayai yasiwe yameyumbishwa yumbishwa sana
6. Mayawe yasiwe na nyufa nyufa
7. Kuku wanaotaga wasiwe wanaumwa
NB. Mayai ya kienyeji yenye Ganda jeupe utotolekaji wake upo chini kidogo kuliko yenye rangi nyingine. Sababu ni kuwa mayai meupe yana calcium nyingi zaidi hivyo Ganda Huwa ni gumu zaidi ukilinganisha na mayai mengine

KARIBUNI SANA MUDA WOWOTE NAFASI IPO 0756282827

SHAMBANI KWETU LEO:Usombaji wa chakula Cha bsf larvae SHAMBANI kwetu. Kwa wale wanaohitaji kufuga nchi chuma ( black sol...
28/06/2026

SHAMBANI KWETU LEO:
Usombaji wa chakula Cha bsf larvae SHAMBANI kwetu. Kwa wale wanaohitaji kufuga nchi chuma ( black soldier flies) kwa ajili ya kupunguza gharama za chakula karibuni 0770903809

26/05/2026

SHAMBANI KWETU LEO:
Hii ni incubator ya mayai 1056. Ni two in one; incubator na hatcher yake. Ni automatic na ukiipata utatumia wewe mpaka mjukuu. Ufanisi wake n mzuri sana. Incubator hii ina jumba la bati siyo mbao. Karibuni
0756282827

SHAMBANI KWETU LEOWale wanaohitaji incubator ya mtindo huu.Hii ni incubator ambayo ufanisi wake ni mpaka 90%Hii ni ya mt...
04/01/2026

SHAMBANI KWETU LEO
Wale wanaohitaji incubator ya mtindo huu.
Hii ni incubator ambayo ufanisi wake ni mpaka 90%
Hii ni ya mteja na imeelekea Kagera.
Karibuni sana.
0756282827

SHAMBANI KWETU LEOMAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKEKila ugonjwa huwa na dalili zake kuu ambazo hutofautisha n...
25/12/2025

SHAMBANI KWETU LEO
MAGONJWA MAKUU YA KUKU, DALILI, NA TIBA ZAKE
Kila ugonjwa huwa na dalili zake kuu ambazo hutofautisha na magomjwa mengine, ingawa zipo zile za kufanana mfano kutokula vizuri, kushusha mabawa, kuzubaa/kusinzia na joto kuwa juu

NEWCASTLE /KIDERI / MDONDO
Dalili kuu: Kupindia shingo juu au chini, mwendo wa kuzungukazunguka, kutembea mwendo wa kurudi nyuma huku kichwa kikiwa kimepindia chini au juu. Dalili isiyo kuu ni mharo rangi ya kijani
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba. kinachotibika ni hizo dalili tu ila ugonjwa hubaki kwenye damu hivyo tumia Trimazine 30% na mult vitamin.

GUMBORO / INFECTIOUS BURSAL DISEASE.
Dalili kuu:Kuharisha rangi nyeupe k**a chokaa. Ukimpasua baada ya kufa kunakuwa na k**a matone ya damu kifuani na kwenye firigisi sehemu ya mbele
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.

MAREK'S DESEASE/ MAHEPE
Dalili kuu:kuparalyse /kukak**aa and kwa miguu na mabawa, Hapa mguu mmoja mara nyingi huwa mbele na mwingine nyuma, kuvimba kwa kihifadhia chakula (crop), kwa kuku wa mayai huathiriwa wakiwa wadogo ila madhara hutokea wakifikisha miezi 5 wakianza kutaga.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba.

NDUI YA KUKU / FOWL POX.
Dalili kuu:Vipele sehemu zisizokuwa na manyoya k**a vile vilemba vya kichwani (comb na wattle), puani na miguuni.
Tiba:Ugonjwa huu husababishwa na virusi kwa hiyo hauna tiba., kupunguza madhara waoshe kwa maji ya uvugu vugu yenye chumvi ya mawe hadi Vipele viishe au vipake mafuta na mpe antibiotic k**a Otc 20%.

MAFUA MAKALI/ INFECTIOUS CORYZA
Dalili kuu:Chafya, kusinzia, kuvimba sehemu za uso, kichwa na macho, ute mzito mweupe jichoni hupelekea jicho kuziba, udenda puani na mdomoni.
Tiba: Fluban, au Tylodox au OTC 20 %, Tylosan, changanya na mult vitamin.

FOWL TYPHOID/ HOMA YA MATUMBO
Dalili Kuu:Mharo rangi ya njano.
Tiba: Esb3, Trimazine 30%, Tylodox.

COCCIDIOSIS/ MHARO DAMU.
Dalili kuu: Kinyesi/mharo rangi ya ugoro mwanzo na unavyoendelea kinakuwa rangi ya damu.
Tiba: Amprolium 20%,Esb3, Trimazine 30%, Vitacox, na Agracox.

FOWL CHOLERA/ KIPINDUPINDU CHA KUKU.
Dalili kuu: kinyesi mharo wa kijani.
Tiba: Trimazine 30 % au Esb3.

MAGONJWA MATATIZO YANAYOTOKAN NA LISHE DUNI
Kuvimba macho, miguu kukosa nguvu na kashindwa kusimama au kutembea, kutaga mayai tepetepe, kula mayai, kudonoana.
Tiba: Chakula kiwe na mchanganyiko mzuri wa mult vitamin na protein, kwa wanaodonoana kata au choma midomo yao na uwape mboga za majani ukiwa umezining'iniza juu kidogo.

K**a utawapa kuku wako wa wanaotaga mayai dawa zenye sulphur ndani watapunguza kutaga mayai, kwa hiyo k**a utaweza kupata dawa ambayo haina sulphur ndani yake itakuwa ni vizuri zaidi

Address

TAGAMENDA, IRINGA
Iringa

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tagamenda Poultry and Egg Incubator Construction Unit posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Tagamenda Poultry and Egg Incubator Construction Unit:

Shortcuts

Share