06/10/2026
UNAJUA KWANINI HUWA TUNATUMIA NGUZO ZA 230 KWA 600 BADALA YA 230 KWA 230?
Matumizi ya nguzo ya 230 mm kwa 600 mm badala ya 230 mm kwa 230 mm hutokea wakati jengo linapokabiliwa na ongezeko kubwa la uzito, umbali mkubwa kati ya nguzo na nguzo, au mahitaji ya kiusanifu namaanisha kutimiza kile ambacgo designer amependekeza.
Kitaalamu, tunabadilisha kwenda ukubwa wa 230x600 katika mazingira yafuatayo:
1. Umbali Mkubwa Kati ya Nguzo (Long Span Beams)
Nguzo ya 230x230 inafaa tu k**a nafasi kutoka nguzo moja hadi nyingine ni fupi sana (isiyozidi mita 3.0 hadi 3.5). K**a (beam) ina urefu mkubwa (span ya mita 5.5 hadi 6.5 au zaidi), uzito unaokuja kwenye nguzo unaongezeka sana. Nguzo inahitaji kuwa ndefu upande mmoja (600 mm) ili kuzuia isipinde au kupasuka kutokana na nguvu ya mgandamizo (shear stress).
2. Idadi Kubwa ya Gorofa (Multi-Storey Buildings)
• Nguzo ya 230x230: Inaruhusiwa tu kwa nyumba ya chini (G+0 / Single-storey) au gorofa moja au mbili yenye mizigo miepesi.
• Nguzo ya 230x600: Inatumika pale jengo linapokuwa la gorofa 3 hadi 5 (G+3 au G+4).
Kadiri ghorofa zinavyoongezeka, uzito wa mrundikano (cumulative axial load) kutoka kwenye slabs za juu unahitaji eneo kubwa zaidi la zege na nondo ili kuhimili mgandamizo.
3. Kuficha Nguzo Ndani ya Ukuta (Aesthetic / Architectural Reasons)
Hii ni siri kubwa ya kiusanifu. Unapojenga ukuta kwa tofali za inchi 9 (ambazo ni sawa na 230 mm):
• Ukitumia nguzo ya mraba mkubwa (k**a 400x400 au 500x500), nguzo itatokeza nje ya ukuta na kuharibu muonekano wa ndani ya chumba au korido.
• Ukitumia 230x600, upande wa 230 mm unazama kabisa ndani ya unene wa tofali (ukuta unabaki umenyooka bila uvimbe), huku urefu wa 600 mm ukiwa umelala kufuata mstari wa ukuta. Hii inakupa nguvu kubwa ya jengo huku ukuta ukiwa msafi na bapa.
4. Kuhimili Bending Moments & Wind Loads
Kwenye majengo marefu au maeneo yenye upepo mkali, jengo halikabiliwi na uzito wa kushuka chini tu (axial load). Linakabiliwa pia na nguvu za kulisukuma kwa pembeni (lateral loads/bending moments).
Upande wa 600 mm unawekwa kuelekea uelekeo wa nguvu hiyo ili kuongeza uimara wa jengo (resisting buckling and bending)….engineering is interesting✋🏻