Mori health clinic

Mori health clinic Afya ni mtaji wa kila mwanadamu Mori health clinic tunajali afya yako

BAWASIRI/KIKUNDU (HAEMORHOIDS)BAWASIRI NI NINI?Ni mkusanyiko wa damu ndani ya njia ya haja kubwa (mkundu na puru) katika...
12/08/2025

BAWASIRI/KIKUNDU (HAEMORHOIDS)

BAWASIRI NI NINI?
Ni mkusanyiko wa damu ndani ya njia ya haja kubwa (mkundu na puru) katika sinusoid za ateri na vena za njia ya haja kubwa. Ikumbukwe kwamba mifumo hii ya damu ni ya kawaida na kila binadamu anazo. Mifumo hio ya damu ya ndani ya njia ya haja kubwa ikijaa damu ndipo inavimba na inakua bawasiri au vijivimbe laini ndani ya njia hiyo. Watu wengi sana wana bawasiri na kwa kua hazinaga dalili basi hata watu wengi hawajijui k**a wana hali hii.Bawasiri huwapata sana watu kuanzia miaka 30 hadi 65;chini ya miaka 20 au juu ya miaka 70 ni ngumu sana kupata bawasiri. Ikumbukwe kwamba bawasiri zipo sana na k**a hazikupi shida yeyote wala hazihitaji matibabu ya aina yeyote

AINA ZA BAWASIRI

👉BAWASIRI ZA NDANI(INTERNAL HAEMORHOIDS)

👉BAWASIRI ZA NJE(EXTERNAL HAEMORHOIDS)

👉BAWASIRI MCHANGANYIKO(MIXED HAEMORHOIDS)

WALIOPO KWENYE HATARI YA KUPATA BAWASIRI

👉Wanaoharisha sana(diarrhea)

👉Wajawazito( pregnancy)

👉Wanaopata choo kigumu kwa muda mrefu(chronic constipation)

👉Wanaokaa muda mrefu kwenye kiti( prolonged sitting)

👉Watu wenye kiribatumbo(obesity)

👉Wanaofanya mapenzi ya njia ya haja kubwa(a**l in*******se)

👉Wanaonyanyua vitu vizito(Regular heavy lifting)

👉Watu wenye maisha mazuri na wasomi(Higher socioeconomic status)

👉Waliofanyiwa operesheni ya aina yeyote ya mkunduni(Rectal surgery)

👉Wenye magonjwa ya ini(Hepatic disease)

👉Watu wenye saratani ya utumbo mpana(Colon malignancy)

👉Wenye presha ya puru(Elevated a**l resting pressure)

👉Wenye presha ya Ini(Portal hypertension

ATHARI ZA BAWASIRI
🔹Upungufu wa damu mwilini
🔹Kutokwa na kinyesi bila kijitambua
🔹kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
🔹kupungukia nguvu za kiume (kwa wanaume)
🔹kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
🔹Kupata tatizo la kisaikolojia

NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI

🔹Kula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi
🔹kunywa maji mengi lita sita hadi kumi na mbili kwa siku
🔹Acha kufanya ngono kwa kutumia tundu la haja kubwa (kulawitiwa)
🔹Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.

MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA UGONJWA WA BAWASIRI
➡️matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri, mara nyingi wagonjwa wa bawasiri hupatiwa tiba ya kukatwa kinyama na kushauriwa kuendelea na tiba ya vyakula Lakini tiba huwa haina matokeo mazuri kwasababu baada ya Muda tatizo hujirudia kutokana na kwamba hawajatibu chanzo cha tatizo hivyo tiba nzuri ya bawasiri ni kutumia dawa itakayotibu chanzo cha tatizo huku ukiendelea na tiba ya chakula, MFANO MZURI WA DAWA NI *BODY SYSTEM* na *BAWASIR LIQUID* hizo zinatibu na kuondoa tatizo moja kwa moja kwa muda wa wiki mbili tu hata k**a ulishawahi kufanyiwa upasuaji hivyo ni vizuri kutumia dawa hizo ili kumaliza tatizo pamoja na hayo ni
vyema ukazingatia mambo yafuatayo ili KUEPUKANA na ugonjwa wa bawasiri

ZINGATIA KANUNI YA CHAKULA BORA KWA KUPENDELEA KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA NA NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GLASI SITA HADI 12 KWA SIKU
EPUKA KUTUMIA MUDA MREFU CHOONI

MADHARA YA BAWASIRI
➡️Ugonjwa wa bawasiri una madhara makubwa iwapo hautapatiwa tiba ya uhakika haya ni baadhi ya madhara ya bawasiri

➡️KUPATA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

➡️KUPATA TATIZO LA KUSHINDWA KUHIMILI KINYESI

➡️HUPUNGUZA MORAL YA KUFANYA KAZI KUTOKANA NA MAUMIVU

➡️HUATHIRI KISAIKOLOJIA
MWANAMKE HUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA

➡️KUPATA KANSA YA YTUMBO
✍ hayo ni mambo ya msingi sana kuyajua kabla ya kujua tiba wa.me/255686110830

UGONJWA WA MSHIPA WA NGIRI (HERNIA/HYDROCELE)Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au ku...
06/08/2025

UGONJWA WA MSHIPA WA NGIRI (HERNIA/HYDROCELE)

Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji. Ugonjwa huu wa ngiri unawapata wanaume na wanawake wa rika zote. Mshipa wa ngili ni jina linalokusanya magonjwa k**a Ngiri kavu (Hernia), Ngiri maji (Hydrocele) na Ngiri nyinginezo k**a vile kuvimba kokwa au mfereji unaopitisha manii unaojulikana kitaalamu k**a Epididmorchitis.

Ngiri Kavu (Hernia), aina hii ya ngiri huwapata wanawake na wanaume wote kwa ujumla. Ngiri kavu inapompata Mwanamke huitwa Fermoral Hernia, na pindi inapompata mwanaume inaitwa Scrotal hernia. Kwa maana halisi ya ngiri au mshipa wa ngiri ni hali inayotokea katika mwili wa binadamu ambapo sehemu fulani ya nyama ya viungo mbalimbali vya mwili hujipenyeza kupitia sehemu dhaifu ya mwili na kutokeza upande wa pili. Sehemu hiyo inayoathiriwa mara nyingi huwa ni maeneo ya tumbo, kokwa, pumbu na kadhalika ambapo baadhi ya viungo vya mwili vilivyomo tumboni hujipenyeza kupitia vitundu vinavopitisha mishipa ya fahamu inayohudumia kokwa (Spesmatic Cord), hivyo baada ya kujipenyeza huteremka hadi ndani ya korodani hali ambayo hukamilisha kuwepo kwa ugonjwa wa mshipa wa ngiri.

Pamoja na hivyo mshipa wa ngili hujitokeza sehemu mbalimbali za mwili na hupewa majina tofauti kutokana na sehemu ulipojitokeza, kwa mfano ngiri ya tumbo inajulikana kitaalamu k**a Abdominal Hernia, pia watoto wanaozaliwa na vitovu vikubwa inaitwa Umbilical Hernia, na pale ngiri inapojitokeza katika sehemu ya haja kubwa inaitwa A**l Herni. Dalili zake hazitofautiani sana hata hivyo ngiri hujitokeza bila maumivu yoyote isipokuwa kuna baadhi ya ngili hujitokeza na maumivu makali hutegemea ngiri ilivotokeza.

Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa wa mwili wa kupitiliza au kuongezeka uzito kwa ghafla, pia kua na kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua.

Mojawapo ya dalili za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;
• Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu k**a Direct Scoratal inguinal Hernia.
• Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.

• Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
• Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.
Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika

======

Ugonjwa wa ngiri ya kitovu (Umbilical Hernia)

Hili ni tatizo la kiafya ambalo huathiri ukuta wa tumbo na kitovu. Tatizo hili husababishwa na mambo makubwa matatu; kwanza ni kasoro ya kuzaliwa. Hapa ni kwamba kitovu kinakuwa na kasoro tangu pale mtoto anapokuwa tumboni kabla hajazaliwa.

Tatizo hili kwa watu wazima lipo mara tatu zaidi kwa wanawake ukilinganisha na wanaume ambapo lipo kwa kiasi kidogo sana. Kwa watoto kiwango cha tatizo hili vinalingana kwa wote wa k**e na wa kiume na tafiti zinaonesha kwamba, tatizo ni kubwa kwa watoto wa Kiafrika ukilinganisha na mataifa mengine.

Aina ya pili ya tatizo hili ni ngiri ya kitovu. Hii inatokea tu pasipo na kasoro za kuzaliwa nazo. Hili linatokea kutokana na shinikizo la mgandamizo wa hewa na nguvu ndani ya tumbo kunakosababishwa na unene kupita kiasi, kunyanyua mizigo mizito au vitu vizito mara kwa mara, kikohozi cha muda mrefu na ujauzito wa mimba ya mapacha kwa mwanamke.

Aina ya tatu ya ngiri ya kitovu inaitwa ‘Paraumbilical hernia’. Aina hii ya ngiri hutokea zaidi kwa watu wazima na husababishwa na kasoro upande wa juu wa kitovu kuelekea kwa juu kufuata mstari wa kati wa tumbo.

DALILI ZA UGONJWA
Ngiri hutokea katika eneo la kitovu ambacho kwa lugha nyingine huitwa ‘Umbilicus’, ‘navel’ au ‘Belly button’. Kwa watoto wachanga wanapozaliwa kitovu huwa kirefu sana na huungana na kondo la nyuma la mama ili kupeleka lishe na hewa ya oksijeni kwa mtoto anapokuwa tumboni.

Baada tu ya kuzaliwa, mtoto hujitegemea hivyo kitovu hukatwa katika eneo maalum ili kipungue urefu. Baada tu ya kitovu cha mtoto kupona, mtoto anaweza kupatwa na tatizo hili la ngiri ya kitovu tangu anapokuwa mtoto mchanga ambapo akilia kitovu kinatokeza juu na anaponyamaza kinarudi ndani.

Hali hii wakati mwingine humsababisha mtoto apatwe na maumivu makali huku akilia kila wakati.

Aina hii ya ngiri huwa haipasuliwi kwani huisha yenyewe baada ya miaka miwili hadi mitatu, lakini baada ya umri huo k**a haikuisha basi mtoto atafanyiwa upasuaji kurekebisha.

Endapo mtoto ngiri hiyo itakuwa inamsumbua kabla ya umri wa miaka mitatu, basi hatapasuliwa bali itafanyiwa utaratibu wa kuirudisha kitaalam ili isiendelee kutokeza na kuleta maumivu. Ngiri inapokuwa kubwa, tundu lake huwa haliongezeki hivyo husababisha matumbo na kila kitu kitachomoza na kubana nje kushindwa kurudi ndani na kusababisha hali iitwayo ‘Strangulation’.

K**a hali hii haitatibiwa mapema basi italazimika upasuaji wa dharura na ikichelewa huweza kuhatarisha maisha ya mgonjwa. Tatizo hili hutokea hata kwa ngiri nyingine ambazo tutakuja kuziona katika matoleo mengine.

UCHUNGUZI
Ngiri ya kitovu huonekana kwa macho pale inapochomoza ambapo dhahiri itaonesha imechomoza, wakati mwingine mgonjwa atalalamika maumivu na k**a ni mtoto atakuwa a**lia mara kwa mara.

Vipimo ni muhimu kwan inasahidia kujua k**a imeleta madhara mengine kwa mawasiliani wa.me/255686110830

*DALILI ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME*```Mwanaume anayekabiliwa na tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume huony...
05/08/2025

*DALILI ZA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME*
```Mwanaume anayekabiliwa na tatizo la ukosefu ama upungufu wa nguvu za kiume huonyesha dalili zifuatazo:-```

```1⃣. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake barabara.
-Kwa kawaida uume wa mwanaume aliyekamilika (rijali ) unaposimama, hutakiwa kuwa imara k**a msumari, lakini kwa mwanaume anaye kabiliwa na tatizo hili uume wake hata ukisimama hubakia kuwa lege lege na huweza kusinyaa wakati wowote. Tatizo hili ni matokeo ya kulegea kwa mishipa ya uume. Mishipa ya uume ndio inayo ufanya uume usimame barabara.

2⃣ .kutokuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa mara moja.
-Hii husababishwa na kutokuwa na msukumo mzuri wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume

3⃣. Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa.
-Hili ni matokeo ya kuwa na msongo wa mawazo.

4⃣. Kufika kileleni mapema

5⃣. Kutokuwa na uwezo wa kusimamisha kabisa.
-Hali hii hutokea pindi tatizo la kutokuwepo kwa msukumo wa damu wa kutosha kwenye mishipa ya uume linapokuwa limekomaa.

6⃣ .Uume kusinyaa na kurudi ndani.
-Hapa uume wa mwanaume unakuwa umesinyaa na kurudi ndani. Uume huu unakuwa hauna uwezo wa kukamilisha tendo la ndoa hali hii husababishwa na upigaji punyeto kw a mda mrefu pia magonjwa hasa chango lá kiume au ngiri.

*SULUHISHO LA UZAZI*
_Msaidie mpenzi wako kumpatia suruhisho la kudumu. Wasiliana nami kwa sim namba wa.me/255686110830

Madhara ya Shinikizo la Juu la DamuShinikizo la Juu la Damu Husababisha Magonjwa ya Kiharusi/Stroke, Moyo kushindwa kufa...
23/06/2025

Madhara ya Shinikizo la Juu la Damu

Shinikizo la Juu la Damu Husababisha Magonjwa ya Kiharusi/Stroke, Moyo kushindwa kufanya Kazi, Kupungua Kwà Nguvu za Kiume, Kupoteza Uoni au Upofu, Shambulizi la Moyo na Magonjwa ya Figo au Figo Kufeli.

Tatizo la Shinikizo Kubwa la Damu linatibika kabisa. Tuma taarifa zako WhatsApp au piga simu au ujumbe mfupi ukionesha Jina Tatizo lako umri eneo Uliopo na tatizo lina muda Gani kwa namba wa.me/255686110830

Eternal white tea much toothpaste……Hii ni dawa ya meno inayotokana na mimea tiba ya asili ambayo imechanganywa kwa pamoj...
19/06/2025

Eternal white tea much toothpaste……

Hii ni dawa ya meno inayotokana na mimea tiba ya asili ambayo imechanganywa kwa pamoja na kuifanya kua dawa yenye nguvu zaidi na bora kuliko zote. Mimea tiba yake inaweza pia kusaidia kuboresha afya ya ngozi kwa mfano kwa wale wanaosumbuliwa na fangazi wa vidoleni au katika kucha.

Ni dawa nzuri ya kusafisha meno kwa ulinzi kamili wa meno na kinywa chako.
Inasaidia kukuweka fresh na kuwa na harufu nzuri ya kinywa wakati wote. Inasaidia kuuwa wadudu ‘bacteria’ wanaoeneza maradhi ya kinywa na meno. Inasaidia pia kwa wale wanaosumbuliwa na ganzi ya meno na wenye meno mabovu inazuia yasisndelee kuharibuka na kuliwa na wadudu.

Hufanya meno kua meupe zaidi na ya kuvutia hasa kwa wale ambao meno yao yameharibiwa na matumizi ya vitu k**a sigara

Kinga ya BawasiriKuhakikisha unapata choo kilaini husaidia kuzuia bawasiri na kupunguza kujirudia kwa dalili za bawasiri...
18/06/2025

Kinga ya Bawasiri

Kuhakikisha unapata choo kilaini husaidia kuzuia bawasiri na kupunguza kujirudia kwa dalili za bawasiri. Hii huwezekana kwa kula vyakula vyenye nyuzinyuzi (fiber),kunywa maji ya kutosha, kuwa na uzito unaofaa, kuepuka kukaa kwa muda mrefu, kuepuka kujikamua wakati wa haja kubwa na kuepuka kubeba vitu vizito mara kwa mara.

Bawasiri ni hali inayoweza kukera lakini mara nyingi hazina madhara mabaya kwa afya ya binadamu. Ugonjwa huu unaweza kuisha wenyewe ndani ya wiki. Bawasiri mara nyingi hujirudia, na hali huzidi kuwa mbaya kadiri muda unavyosonga mbele. Bawasiri ni tatizo la kawaida ambalo linaweza kuathiri watu wengi wakati fulani maishani mwao. Kwa bahati nzuri, kuna hatua ambazo mtu anaweza kuchukua kuboresha hali hii au kuzuia kujirudia. Kwa mfano, kuhakikisha ulaji wa chakula chenye ufumwele (fiber) mwingi na kunywa maji ya kutosha kunaweza kusaidia kuzuia tatizo la bawasiri.

Ili kupunguza dalili za bawasiri, unaweza kujaribu matibabu ya nyumbani k**a vile kujikanda kwa barafu ili kupunguza uvimbe au kutumia dawa za kupunguza maumivu. Hata hivyo, ni muhimu kushauriana na daktari ikiwa dalili zinazidi kuwa mbaya au nafuu haijapatiakana baada ya muda mfupi ili kupata ushauri na matibabu sahihi.

Matibabu ya BawasiriBawasiri inatibika na kuna njia mbalimbali za kutibu bawasiri. Tiba halisi ya bawasiri ni kuhakikish...
18/06/2025

Matibabu ya Bawasiri

Bawasiri inatibika na kuna njia mbalimbali za kutibu bawasiri. Tiba halisi ya bawasiri ni kuhakikisha kupata choo kilaini na kuepuka kufunga choo, ili kuepuka hali kuwa mbaya zaidi. Krimu za kupaka na dawa za kuingiza katika njia ya haja kubwa (suppositories) zinaweza kusaidia kupunguza uvimbe, mwasho na maumivu. Dawa hizi hupatikana katika maduka ya dawa. Kuna matibabu mengine ambapo sindano au kamba maalum hutumika ili kupunguza ukubwa wa mishipa ya damu. Zipo dawa zakukusaidia kutibu bawasiri bila upasuaji.
Kwa mawasiliano ushauri elimu na tiba wasiliana nami wa.me/255686110830

Utambuzi wa BawasiriUtambuzi hufanywa na daktari kwa kuchukua maelezo ya mgonjwa na kuchunguza njia ya haja kubwa. Uchun...
18/06/2025

Utambuzi wa Bawasiri

Utambuzi hufanywa na daktari kwa kuchukua maelezo ya mgonjwa na kuchunguza njia ya haja kubwa. Uchunguzi wa njia ya haja kubwa hujumuisha kuangalia eneo hili na kuingiza kidole taratibu kuchunguza sehemu ya ndani ya njia ya haja kubwa. Ikiwa bawasiri hazionekani kirahisi, au sababu ya kutoka damu haijaeleweka vizuri, uchunguzi wa ziada huweza kufanywa ili kuhakikisha hamna sababu nyingine ya dalili hizi.

Kwa mawasiliano ushauri tiba na elimu wasiliana nami wa.me/255686110830

Address

Nasra Tower Kariakioo Gerezanin
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mori health clinic posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share